Pata taarifa kuu
CAR-WAKIMBIZi-USALAMA

Wakimbizi Jamhuri ya Afrika ya Kati: Kurudi nchini haimaanishi mwisho wa wa matatizo

Watu milioni ishirini na sita ni wakimbizi kote ulimwenguni. Mwaka huu ni hali isiyo ya kawaida, kwa sababu ya mgogoro wa kiafya uliosababishwa na janga la Corona. Hata hivyo bado kuna wakimbizi zaidi ya 600,000 kutoka Afrika ya Kati, hasa nchini Cameroon na DRC wanaosubiri kurejea nchini.

Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati huko Bertoua, mashariki mwa Cameroon.
Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati huko Bertoua, mashariki mwa Cameroon. AFP PHOTO/STR
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR linafanya juhudi hasa kusaidia wakimbizi hao kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambao mara nyingi walikimbia vurugu na vita kurudi nchini. Mnamo mwaka wa 2019, watu 12,500 walirudi nchini Jamhuri ya afrika ya Kati kwa hiari yao.

Reno aliondoka Bangui mnamo mwaka 2013 wakati mji alikokuwa akiishi ulikumbwa na machafuko. Mwezi Desemba 2019 aliamua kurejea katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya kati. "Siwezi kuwa mkimbizi wa milele. Hali kidogo ni ngumu. Sasa kwa kuwa nimerudi, nimekuwa kama mgeni. Nyumba yangu iliharibiwa na waasi wa zamani wa Seleka. Kwa sasa ninajikuta katika maisha yangu yaanza mwanzo. Kwa hivyo sina budi ya kukodisha nyumba kwa sasa, amesema."

Wakimbizi wanaorejea nchini ni wale kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui na magharibi mwa nchi. Kama huko Berberati, Youssouf alirejea nchini mnamo mwaka 2018 baada ya kukimbilia nchini Cameroon miaka minne iliyopita. "Nilipata shida niliporudi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwanza nilipata shida kwa utaratibu uliowekwa kwenye mpaka. Wakati nilipofika hapa, hali ilikuwa ngumu, kwa nyumba nilikuta iliharibiwa na mali zikaibwa, "amesema.

Kuishi na watu waliotokea ukimbizini haikuwa rahisi. "Kuna watu, wakimbizi wa ndani waliokuja kuishi katika nyumba zetu. Nilipokuja nyumbani kwangu, nilichukuliwa kama mgeni kwa hivyo na mimi mwenyewe niliwaona kama wageni. Kutokana na hali hiyo, kuna shirika moja lisilo la kiserikali lilikuja kutupatanisha na kuboresha maridhiano. Kwa kweli ilikuwa ngumu sana, " ameongeza Bw; Youssouf.

Wakimbizi wanaorejea makwao wapata shida nyingine kubwa kwa kupata ajira na kukidhi maisha yao kutokana na janga la Corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.