Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

Jenerali Pino Pino na Kevin Béré-Béré wahukumiwa kifungo cha maisha na kufanya kazi ngumu

Washtumiwa katika kesi inayojulikana kama Bangassou wamehukuliwa leo na mahakama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Wahusika wakuu kutoka kundi la zamani la wanamgambo wa Kikiristo, Anti-balaka, wamehukumiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Wakimbizi Waislamu karibu na msikiti wa Bangassou CAR, Agosti 14, 2017.
Wakimbizi Waislamu karibu na msikiti wa Bangassou CAR, Agosti 14, 2017. Alexis HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Washtumiwa hao wakuu, ikiwa ni pamoja na Jenerali Pino Pino na Kevin Béré-Béré, wamehukumiwa kifungo cha maisha na kufanya kazi ngumu.

Wapiganaji wengine waliopatikana na hatia wamehukumiwa kifungo cha miaka 10 hadi 15.

Katika kesi hiyo, ambayo ilidumu zaidi ya wiki tatu, washtumiwa thelathini wameshtakiwa kwa machafuko yaliyotekelezwa mnamo mwaka 2017 huko Bangassou, jiji linalopatikana Kusini mwa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, machafuko ambayo yaligharimu maisha ya watu wengi, ikiwa ni pamoja na Walinda amani na kusababisha watu wengi kuyatoroka makaazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.