Pata taarifa kuu
DRC-KAMERHE-UCHUMI-HAKI

Mpango wa siku 100 DRC: Mpwa wa Vital Kamerhe akabidhiwa mahakama

Daniel Masaro, mpwa wa Vital Kamerhe, ambaye amekabidhiwa vyombo vya sheria Jumatatu wiki hii, baada ya kusakwa kwa mwezi mmoja, na kupatikana mwishoni mwa wiki iliyopita, anatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama Jumatatu ya wiki ijayo.

Vital Kamerhe alikuwa akisimamia mpango wa dharura wa siku 100 ambao umemtia matatani na kutuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umaa.
Vital Kamerhe alikuwa akisimamia mpango wa dharura wa siku 100 ambao umemtia matatani na kutuhumiwa matumizi mabaya ya fedha za umaa. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na chanzo cha polisi, Daniel Masaro alikuwa amejificha katika shamba linalopatikana nje ya mji wa Kinshasa, mashariki mwa mji mkuu. Hapo ndipo polisi walikwenda kumdhibiti na kumkamata Ijumaa ya wiki iliyipita.

Jumatatu alasiri Mei 18 Daniel Shangalume Masaro alikabidhiwa ofisi ya mashtaka katika wilaya ya Matete jijini Kinshasa.

Kulingana na vyanzo vingine kutoka ofisi ya mashitaka, Jumanne hii atasikilizwa na mwendesha mashitaka.

Daniel Shangalume Masar anashukiwa kumkutanisha mkurugenzi wa ofisi ya rais Tshisekedi na mfanyabiashara kutoka Lebanon Samih Jammal katika shughuli kuhusu mkataba wa ujenzi wa nyumba na kunufaika kwa matumizi mabaya ya fedha za umma katika sehemu ya mpango wa siku 100 wa rais Felix Tshisekedi. Kesi ambayo inawakabili mjomba wake Vital Kamerhe na Samih Jammal.

Daniel Shangalume Nkingi, alias Massaro, amepatikana nje kidogo ya mji mkuu Kinsaha karibu na eneo la Bateke.

Shangalume Nkingi ambaye anahusika na masuala ya tathmini katika Wizara ya Bajeti, alipotea siku ambayo alikuwa anatarajiwa kusikilizwa na ofisi ya mashitaka ya wilaya ya Matete jijini Kinshasa, Aprili 9, siku moja baada ya kukamatwa kwa mjomba wake.

Vital Kamerhe anatuhumiwa kupitisha mlango wa nyuma zaidi ya dola milioni 50 kwa jumla ya dola Milioni 500 zilizotengwa kwa mpango wa rais wa "siku 100" .

Kesi ya Vital Kamerhe iliahirishwa hadi Mei 25 mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.