Pata taarifa kuu
DRC-KAMERHE-HAKI-UCHUMI

DRC: Vital Kamerhe na washtakiwa wenzake wasalia jela

Ombi la Vital Kamerhe na washtakiwa wenzake kuachiwa huru kwa dhamana lililotolewa na wanasheria wao limefutiliwa mbali na majaji wa mahakama ya Gombe, kulingana na hati iliyotolewa mahakama hiyo Jumanne wiki hii.

Vital Kamerhe, mkurugenzi mkuu wa ofisi ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi.
Vital Kamerhe, mkurugenzi mkuu wa ofisi ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Vital Kamerhe na washtakiwa wenzake wanaendelea kuzuiliwa katika jela kuu la Makala, jijini Kinshasa, kwa mujibu wa Radio ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, Okapi, ikinukuu vyanzo kutoka mahakama.

Kesi ya Vital Kamerhe na washtakiwa wenzake, Jammal Samil na Jeannot Muhima ilisikilizwa kwa dadika chache kabla ya kuahirishwa Jumatatu Mei 11 katika gereza kuu la Makala.

Bw. Kamerhe anashtumiwa kupitisha mlango wa nyuma asilimia kumi ya Dola milioni 500 zilizotengwa kwa mpango huo wa siku mia moja wa rais Felix Tshesekedi.

Hata hivyo Mawakili wake Kamerhe wameendelea kukanusha tuhuma dhidi ya mteja wao.

Kulingana na madai ya mwendesha mashtaka, Vital Kamerhe na mfanyabiashara kutoka Lebanon Samih Jammal, kati ya mwezi Machi 2019 na mwezi Januari 2020, walipitisha mlango wanyuma karibu Dola milioni 49. Wawili wanakabiliwa na kifungo hadi miaka ishirini.

Kesi ya Vital Kamerhe na washtakiwa wenzake iliahirishwa hadi Mei 25.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.