Pata taarifa kuu
DRC-KAMERHE-HAKI-UCHUMI

Kesi ya Vital Kamerhe kuanza kusikilizwa Mei 11

Kesi inayomkabili mkurugenzi wa afisi ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasio ya Congo, Vital Kamerhe imepangwa kusikilizwa ifikapo Mei 11 kufuatia tuhuma dhidi yake kuhusu matumizi mabaya ya pesa za serikali.

Vital Kamerhe, kiongozi wa chama cha UNC, Septemba 1, 2016.
Vital Kamerhe, kiongozi wa chama cha UNC, Septemba 1, 2016. JUNIOR D.KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa barua ya mahakama, mbali na mkurugenzi huyo wa afisi ya rais Vital Kamerhe, kesi hii itawashirikisha washtakiwa wengine wawili, Samih Jammal, msimamizi mkuu wa kampuni Samibo Congo Sarl na Husmal Sarl, kampuni ya mafundi wa ujenzi kutoka Uturuki Karmod inayojihusisha na ujenzi wa makazi.

Inadaiwa kwamba Kamerhe pamoja na Samih Jammal, walikubaliana kujenga zaidi ya makazi ya jamii elfu 4,500 katika majimbo matano, na pia kuboresha hali ya makazi ya polisi na wanajeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa.

Samih Jammal, mkuu wa afisi ya rais wa DRC, Pamoja na mshtakiwa wa tatu  Jeannot Muhima wanatuhumiwa kutumia zaidi ya dola milioni 50 kati ya milioni 60 zilizotengwa kati ya mwezi Machi na Agosti 2019 katika mpango wa siku 100 wa rais Felix Tshisekedi.

Majaji wa mahakama hiyo jijini Kinshasa pia wanamtuhumu Vital Kamerhe kwa kumshirikisha shemeji yake Soroya Mpiana, katika makubaliano ya ununuzi wa uwanja kati yake na msimamizi mkuu wa kampuni Samibo Congo, Samih Jammal.

Kesi hii itasikilizwa siku ya Jumatatu Mei 11, katika ukumbi wa Mahakama, wakati huu mawakili wake Vital Kamerhe wakiendelea kukanusha tuhuma dhidi ya mteja wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.