Pata taarifa kuu
ALGERIA-UCHUMI-HAKI

Mtoto wa rais wa Algeria Tebboune afikishwa mahakamani

Kesi ya Kamel Chikhi, mfanyabiashara aliyehusishwa katika kesi ya biashara ya madawa ya kulevya imeanza. Lakini kuwepo kwa mmoja wa washtakiwa wenzake mahakamani, Khaled Tebboune, kumezua hisia tofauti. Naye si mwingine ni mtoto wa rais wa sasa wa Algeria Abdelmadjid Tebboune.

Rais mpya wa Algeria Abdelmadjid Tebboune wakati wa kuapishwa kwake huko Algiers, Desemba 19, 2019.
Rais mpya wa Algeria Abdelmadjid Tebboune wakati wa kuapishwa kwake huko Algiers, Desemba 19, 2019. RYAD KRAMDI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu kuchaguliwa kwa Abdelmadjid Tebboune mwezi Desemba mwaka jana, watumiaji wa mtandao na waandamanaji walimdhihaki, "rais wa Cocaine". Maneno ambayo yalikemea utaratibu wa mahakama kuhusu kesi ya mtoto wake, Khaled Tebboune.

Khaled Tebboune anashtumiwa kuwa na uhusiano na Kamel Chikhi anayekabili na mashitaka.

Kamel Chikhi ndiye mtuhumiwa mkuu katika kesi ya hii ihusuyo kilo 700 za madawa ya kulevya aina ya Cocaine zilizokamatwa katika bandari ya Algeria mnamo mwezi Mei 2018.

Lakini wakati wa uchunguzi, kufika kwa Khaled Tebboune katika ofisi za Kamel Chikhi kuliwashangaza wengi. Wachunguzi wanashuku kwamba mtoto wa rais Tebboune anahusika katika kesi nyingine inayohusu miradi ya mali isiyohamishika.

Hivi sasa akiwa kizuizini na washtakiwa wengine sita, Khaled Tebboune atakabiliwa na mashtaka kadhaa, pamoja na "kufanya biashara kwa ushawishi", "utumiaji mbaya wa madaraka", "ukusanyaji wa zawadi zisizofaa" na "ufisadi".

Aliwekwa kizuizini mnamo mwezi Juni 2018, mwaka na nusu kabla ya uchaguzi wa baba yake kama rais wa Algeria. Abelaziz Bouteflika wakati huo alikuwa bado rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.