Pata taarifa kuu
CHAD-BOKO HARAM-SIASA-NIGERIA

Boko Haram yaua watu 13 Magharibi mwa nchi ya Chad

Watu 14 wameuawa na wengine 13 hawajulikani walipo, baada ya kushambuliwa na wanajihadi wa Boko Haram katika kijiji chenye umaarufu wa uvuvi, Magharibi mwa nchi ya Chad.

Wanajeshi wa Nigeria, wanaopambana na kundi Boko Haram nchini Nigeria
Wanajeshi wa Nigeria, wanaopambana na kundi Boko Haram nchini Nigeria REUTERS/Warren Strobel
Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yametokea katika kijiji cha Kaiga, pembezoni mwa Ziwa Chad, kwa mujibu wa viongozi wa serikali katika eneo hilo.

Kijiji hicho kinapakana na nchi nne, za Cameroon, Chad, Niger na Nigeria.

Ripoti zinasema kuwa, watu wenye silaha walikuja wawache na baadaye kuongeza na kuwashambulia wavuvi. Kwa mujibu wa Gavana wa eneo hilo Noki Charfadine.

Kundi la Boko Haram limeendelea kusababisha mauaji Kaskazini mwa Nigeria na nchi jirani, na kusababisha vifo vya watu 35, 000 na zaidi ya watu Milioni mbili kuyakimbia makwao katika miaka ya hivi karibuni.

Pamoja na Nigeria, tishio la Boko Haram limekwenda katika nchi jirani ya Chad, Cameroon na Niger, mataifa ambayo yameungana kupambana na kundi hilo.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.