Pata taarifa kuu
BOTSWANA-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi nchini Botswana: Chama tawala chakabiliwa na upinzani mkubwa

Kwa mara ya kwanza nchini Botswana, chama kilichopo madarakani tangu uhuru hakina uhakika wa kupata ushindi wa uchaguzi uliopangwa kufanyika Jumatano Oktoba 23.

Mabango ya uchaguzi katika mitaa ya Gaborone, mji mkuu wa Botswana, Oktoba 2019.
Mabango ya uchaguzi katika mitaa ya Gaborone, mji mkuu wa Botswana, Oktoba 2019. © Monirul Bhuiyan / AFP
Matangazo ya kibiashara

Chama cha Botswana Democratic Party (BDP) kinakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka muungano wa upinzani Umbrella for Democratic Change (UDC), ambao unapewa nafasi kubwa ya kushinda.

Jeshi limekataa kutumiwa kama hoja ya uchaguzi, wakati wa kampeni ya uchaguzi yenye ushindani mkubwa nchini Botswana, huku kila upande ukinadi sera yake kwa wafuasi wake.

Mgombea wa muungano wa upinzani, Umbrella for Democratic Change (UDC), amerusha picha za askari kwenye mitandao ya kijamii, ambao amejaribu kutetea mazingira yao ya kazi. Lakini, sheria inabaini kuwa jeshi halina upande wowote linaloegemea katika siasa. Jeshi limekanusha taarifa kutoka upinzani kwamba, linaegemea upande wa chama tawala, kwa kuwa jeshi linamsafirisha rais anayemaliza muda wake katika ndege zake katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Kwa upande wake, Rais Mkgweetsi Masisi mwenye umri wa miaka 58, mtoto wa waziri, mwigizaji wa zamani na mwalimu wa shule ya upili, amesema ana imani kuwa Chama chake cha Botswana Democratic Party (BDP), madarakani tangu Botswana kupata Uhuru mwaka 1966 kitashnda uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.