Pata taarifa kuu
TUNISIA-SIASA-USALAMA

Tunisia: Kampeni ya uchaguzi wa urais kumalizika leo Ijumaa

Kampeni ya uchaguzi wa urais inamalizika leo Ijumaa nchini Tunisia. Wagombea wawili maarufu, Kais Saied na Nabil Karoui, ndio watapambana katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais.

Mmoja kati ya wapiga kura vijana akitumbukiza kura yake katika sanduku la upigaji kura Oktoba 6 Tunis, wakati wa uchaguzi wa wabunge.
Mmoja kati ya wapiga kura vijana akitumbukiza kura yake katika sanduku la upigaji kura Oktoba 6 Tunis, wakati wa uchaguzi wa wabunge. © FETHI BELAID / AFP/ AFP
Matangazo ya kibiashara

Kais Saied, ambaye alipata 18.4% ya kura katika duru ya kwanza, atapambana na mfanyabiashara Nabil Karoui, aliyepata asilimia 15,58. Mapema wiki hii mahakama ilimwachilia huru Bw Karoui, ambaye alikuwa kizuizini tangu Agosti 23 kwa madai ya utakatishaji fedha na ukwepaji kodi. Leo usiku, wagombea wote wawili watashiriki mjadala wa televisheni.

Wananchi wa Tunisia wameanza, kila mmoja, kutoka maoni yake kuhusu uchaguzi huo na kuweka wazi matatizo yanayoikabili nchi yao kwa sasa. Hali ya uchumi iko mashakani nchini humo, idara mbalimbali za umma hazifanyi kazi vilivyo, kunaripotiwa ukosefu wa ajira, na pia mfumko wa bei unaendelea kushuhudiwa nchini humo. wananchi wengi wa Tunisi wanataka hali zao za maisha kuboreshwa.

"Nilifanya kazi kwa miaka 35 katika Wizara ya Vijana," amesema Adel Tounes, mtumishi wa umma aliyestaafu. Ninajitahidi kufanya kazi katika mgahawa huu ili kupata ruzuku. Nina watoto wawili wa kiume: mmoja yuko nje ya nchi, na anafanya kazi katika Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP; mwiengine hana kazi tangu mwaka 2014. Ana nia ya kuondoka nchi hii kwa sababu hapa hakuna matarajio ya vijana. "

Katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais, 9% tu ya vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 25 ndio walipiga kura. Kwa mujibu wa mwanasaikolojia Omar Zafouri, hii inaweza kuwa moja ya sababu ya maswala ya kielimu. "Kadri umri unavyoongezeka, kiwango cha ushiriki kinaongezeka: 9% kwa vijana wadogo, 33% kwa watu wazima, na 57% kwa watu walio na umri wa miaka zaidi ya 50, amesema profesa huyu wa Chuo Kikuu cha Sfax.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.