Pata taarifa kuu
DRC-UN-USALAMA-SIASA

DRC: Hatma ya MONUSCO kugubika mkutano wa Guterres na Tshisekedi

Baada ya ziara yake katika mji wa Goma Jumamosi na Beni Jumapili mwishoni mwa wiki hii iliyopita, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatarajia Jumatatu hii kukamilisha ziara yake mjini Kinshasa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa na makada wa kijeshi wa Umoja wa Mataifa katika kituo cha kuwarejesha wapiganaji katika maisha ya kiraia (DDR), Munigi, Goma, DRC, Agosti 31, 2019.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres akiwa na makada wa kijeshi wa Umoja wa Mataifa katika kituo cha kuwarejesha wapiganaji katika maisha ya kiraia (DDR), Munigi, Goma, DRC, Agosti 31, 2019. © REUTERS/Djaffar Sabiti
Matangazo ya kibiashara

Antonio Guterres anatarajia kukutana kwa mazungumzo na Rais Felix Tshisekedi, lakini pia Waziri Mkuu, Spika wa Bunge la kitaifa na wawakilishi wa upinzaji na asasi za kiraia. Kwenye ajenda ya mazungumzo ya viongozi hao ni pamoja na hatma ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) na mapambano dhidi ya makundi yenye silaha.

Jana katika ziara yake mji Beni, Antonio Guterres alikubali kwamba kuna hitajika "zaidi" mapambano dhidi ya makundi yenye silaha na aliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuongeza muda wa MONUSCO na "marekebisho yaliyo kuwa muhimu" kwa kufanya kikosi hicho cha Umoja wa Matiafa kuwa na "uwezo zaidi", wakati muda tume ya Umoja wa Mataifa utamalizika mwishoni mwa mwezi Desemba.

Antonio Guterres amesema, "MONUSCO ina kazi kubwa nchini DRC". "Kwa kweli siku moja, Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC itafunga milango yake," alisema Antinio Guterres

Hata hivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amebaini kwamba, suala la MONUSCO kuondoka "kuanzia mwaka 2020" kama ilivyodaiwa na rais wa zamani Joseph Kabila ni hatua ya haraka, ambayo haingiweza kuzaa matunda yoyote. Amesema "ana imani na Baraza la Usalama" "kuongeza" muda wa kikosi cha Umoja wa Mataifa mwishoni mwa mwezi Desemba "na kufanya marekebisho muhimu" ili kukifanya "kuwa nguvu zaidi". Na pia ameomba "ushirikiano wa kutosha" kati ya kikosi cha MONUSCO na jeshi la DRCongo katika mapambano dhidi ya makundi yenye silaha.

Katika miaka ya nyuma, wakati wa utawala wa Joseph Kabila, uhusiano kati ya Kinshasa na New York uliingiliwa na dosari, hivyo Umoja wa Mataifa kuamua kupunguza operesheni zake nchini DRC. MONUSCO na FARDC hawajafanya tena operesheni ya pamoja dhidi ya waasi wa ADF tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.