Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA

Mazungumzo kati ya jeshi na viongozi wa maandamano yaahirishwa Sudan

Mazungumzo yaliyopangwa Ijumaa wiki hii kati viongozi wa maandamano na utawala wa kijeshi nchini Sudan ili kukamilisha pointi ambazo pande zote mbili zimekuwa bado zikitafautiana baada ya kumalizika kwa mkataba wa kugawana madaraka, umeahirishwa, kwa mujibu wa viongozi wa maandamano.

Wananchi wa Sudan wakisherehekea katika mitaa ya Khartoum tangazo la makubaliano kati ya jeshi na viongozi wa maandamano ili kukomesha mgogoro, Julai 5, 2019.
Wananchi wa Sudan wakisherehekea katika mitaa ya Khartoum tangazo la makubaliano kati ya jeshi na viongozi wa maandamano ili kukomesha mgogoro, Julai 5, 2019. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

"Mazungumzo yameahirishwa," Omar al-Digeir, mmoja kati ya viongozi wa maandamano, ameliambia shirika la Habari la AFP.

"Tunahitaji mashauriano zaidi ili kufikia msimamo mmoja," amesema, bila kutaja tarehe mpya ya mazungumzo.

Kiongozi mwingine wa maandamano, Siddig Youssef, pia amethibitisha kuahirishwa kwa mazungumzo hayo.

Jumatano, pande hizo mbili zilifikia "tamko la kisiasa", makubaliano ya kugawana madaraka kati ya Baraza la kijeshi lililochukuwa nafasi ya rais aliyepinduliwa madarakani Omar al-Bashir, mwezi Aprili, na viongozi wa maandamano, hatua ya kwanza kuelekea serikali ya kiraia, madai muhimu ya waandamanaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.