Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Tshisekedi azuru mkoa wa Kivu Kaskazini unaokabiliwa na mdororo wa usalama

Ikulu ya rais nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imefahamisha kuwa, Rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi Tshilombo amewasili Jumapili Aprili 14 jijini Goma, mkoa wa Kivu Kaskazini ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kwanza ndani ya nchi tangu kuchaguliwa kwake Mwezi Desemba mwaka jana.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi aendelea na ziara yake katika mikoa mbalimbali ya nchi.
Rais wa DRC Felix Tshisekedi aendelea na ziara yake katika mikoa mbalimbali ya nchi. REUTERS/ Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi anazuru jimbo la Kivu, eneo ambalo limeendelea kukumbwa na utovu wa usalama na maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola.

Ziara hiyo ilianzia mjini Lubumbashi ambako rais Tshisekedia alikutana na viongozi wa sekta mbalimbali katika Mkoa huo.

Baada yakuapishwa kwake kipaombele cha rais Tshisekedi ilikuwa ni ziara za nje kuliko za ndani.

Tangu kuapishwa kwake Januari mwaka huu rais Tshisekedi amesha fanya ziara katika mataifa zaidi ya 5, ikiwa ni pamoja na nchi jirani ya Rwanda na Uganda bila kusahau Kenya ambapo rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta alihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais Tshisekedi mjini Kinshasa.

Tangu kuchaguliwa kwake kuwa rais wa DRC, rais Tshisekedi hajatangaza baraza lake la mawaziri.

Hata hivyo kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na ikulu ya Kinshasa serikali mpya inayotarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.