Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

DRC: Tshisekedi aombwa kutengua uteuzi wa Roger Kibelisa

Wanaharakati wa vyama vya kiraia nchini DRC na wafungwa wa zamani waliokuwa wakizuiliwa na idara ya upelelezi nchini humo (ANR) wamemuandikia barua rais Felix Tshisekedi wakimuomba kutoteua kwenye nafasi mbalimbali watu waliohusika katika ukiukwaji wa haki za binadamu.

Katikati mwa mwezi Machi, rais Tshisekedi alimteua Roger Kibelisa kama Msaidizi wa Mshauri Maalum wa rais katika masuala ya Usalama.
Katikati mwa mwezi Machi, rais Tshisekedi alimteua Roger Kibelisa kama Msaidizi wa Mshauri Maalum wa rais katika masuala ya Usalama. © JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waliotia saini kwenye barua hiyo ya wazi wamelaani hasa uteuzi wa Roger Kibelisa kwenye nafasi ya Msaidizi wa Mshauri Maalum wa rais wa jamhuri katika masuala ya usalama na kumuomba rais Tshisekedi "kuahirisha" uamuzi wake.

Roger Kibelisa ambaye anashikilia nafasi ya juu katika idara ya upelelezi nchini DRC, ni mmoja kati maafisa kumi na nne wanaokabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Ulaya kwa kuhusika kwake katika ukandamizaji wa maandamano ya upinzani kati ya mwishoni mwa mwaka 2016 na 2018, kwa mujibu wa Beni Carbone, mratibu wa shirika la kiraia Filimbi, na mmoja miongoni mwa waanzilishi waliotoa wito huu.

Bw Kibelisa alihusika na ukandamizaji wa watu ambao walikuwa hawaungi mkono muhula wa tatu wa Joseph Kabila.

"Tulikutana ili kumuandikia barua rais aweze kuahirisha uteuzi huo au atengue uamuzi wake" , amesema Carbone Beni, mratibu wa Filimbi

Baadhi wanadai kuwa walifungwa katika mazingira mabaya na idara ya upelelezi katika jela liitwalo 3 zoulou (3Z: sehemu isiyojulikana na vyombo vya sheria vya DRC).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.