Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Serikali mpya yaundwa Algeria, maandamano yaendelea

Serikali mpya nchini Algeria inajumuisha mawaziri ishirini na saba, ikiwa ni pamoja na wanawake sita. serikali hiyo ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa wiki tatu, haijajibu ahadi zilizotolewa.

Noureddine Bedoui anaendelea kuwa waziri mkuu wa serikali mpya ya Algeria, iliyotangazwa Jumapili, Machi 31, 2019.
Noureddine Bedoui anaendelea kuwa waziri mkuu wa serikali mpya ya Algeria, iliyotangazwa Jumapili, Machi 31, 2019. REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Algeria waliahidi kuunda serikali itakayojumuisha wanawake, lakini walioteuliwa ni sita pekee, kati ya mawaziri 28 - ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu. Kuhusu uteuzi wa vijana kwenye nafasi nyeti za serikali mpya, wawili pekee ndio wameteuliwa. Meriem Merdaci, mwenye umri wa miaka 36, ameteuliwa kuwa Waziri wa Utamaduni na Raouf Bernaoui, 43, ameteuliwa kuwa Waziri wa Vijana na Michezo.

Viongozi wengine wa serikali mpya ni maafisa waandamizi katika serikali iliyokuepo na viongozi wa makampuni ya serikali.

Mawaziri wa zamani sita wamesalia kwenye nafasi zao.

Noureddine Bedoui, anaendelea kuwa Waziri Mkuu, naye Jenerali Ahmed Gaïd Salah anaendelea kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa majeshi. Hata hivyo kulingana na taarifa iliyofichuliwa Jumapili hii, Machi 31, 2019, waziri wa Mambo ya Nje, Ramtane Lamamra, amefutwa kazi na nafasi yake imechukuliwa na Sabri Boukadoum.

Licha ya mabadiliko haya, raia wa Algeria wanaendelea kushinikiza kuondoka madarakani wa rais Bouteflika.

Waandamanaji wameendelea kuandamana wakitaka rais Abdelaziz Bouteflika ajiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.