Pata taarifa kuu
OIF-KIFARANSA-JAMII-USHIRIKIANO

Siku ya Kimataifa ya nchi zinazo zungumza Lugha ya Kifaransa yaadhimishwa

Jumuiya ya nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa inaadhimisha siku ya kimataifa ya nchi zinazozungumza lugha hiyo duniani. Kifaransa kwa leo kinazungumzwa na watu takribani milioni 300 duniani, asilimia 60 ni kutoka barani Afrika.

Kulingana na uchunguzi wa OIF, asilimia 60 ya wazungumzaji wa kila siku wa Kifaransa wako katika bara la Afrika (picha: moja ya madarasa ya shule za msingi Niamey, Niger).
Kulingana na uchunguzi wa OIF, asilimia 60 ya wazungumzaji wa kila siku wa Kifaransa wako katika bara la Afrika (picha: moja ya madarasa ya shule za msingi Niamey, Niger). RFI/Alice Milot
Matangazo ya kibiashara

Kila ifikapo March 20 ni siku ya Kimataifa ya nchi zinazo zungumza Lugha ya Kifaransa ama "Journée Interantionale de Francophonie", ni fursa kwa nchi wanachama kote duniani kuandaa matukio mbalimbali ya kijamii na kitamaduni.

Kifaransa ambacho kinazungumzwa katika mabara yote matano, ni lugha ya tano inayozungumzwa zaidi ulimwenguni, baada ya Kichina, Kiingereza, Kihispania na Kiarabu.

Kulingana na utabiri wenye kuaminika, idadi ya wanaozungumza Kifaransa inaweza kufikia kati ya milioni 477 na milioni 747 hadi mwaka 2070.

Ukuaji wa lugha hii unatokana hasa na kuongezeka kwa idadi ya watu barani Afrika ambapo, kwa mujibu wa taarifa ya hivi karibuni ya Jumuiya ya kimataifa ya nchi zinazozungumza Kifaransa, La Francophonie (OIF), Afrika imekuwa nguzo ya La Francophonie.

Kwa leo Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa inaongozwa na Louise Mushikiwabo, waziri wa zamani wa mambo ya Nje wa Rwanda.

Mushikiwabo mwenye umri wa miaka 57, alichaguliwa kuwa katibu mkuu wa jumuiya hiyo baada ya kuungwa mkono na Umoja wa Afrika (AU) na Ufaransa na kumuangusha mpinzani wake Michaelle Jean, raia wa Canada ambaye alikosa uungwaji mkono kutoka kwa viongozi wa Canada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.