Pata taarifa kuu
RWANDA-ARMENIA-OIF-USHIRIKIANO

Mkutano wa OIF: Mushikiwabo ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Francophonie

Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa, Francophonie (OIF), imemteua Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo kuwa Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo. Hatua hiyo imechukuliwa Ijumaa hii , Oktoba 12, 2018 huko Erevan, nchini Armenia.

Louise Mushikiwabo Katibu Mkuu mteule wa Francophie (OIF). Erevan, Oktoba 12, 2018.
Louise Mushikiwabo Katibu Mkuu mteule wa Francophie (OIF). Erevan, Oktoba 12, 2018. LUDOVIC MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Makubaliano yalifikiwa katika kikao cha faragha cha viongozi wa nchi 84 wanachama wa Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa. "Nimekuja katika mkutano wa Erevan kama Mnyarwanda, kutoka Afrika, naondoka kama mmoja wa viongozi wa Francophonie," Loiuse Mushikiwabo amesema.

Kifungu kinasasishwa mara kwa mara na mwandishi wetu maalum katika Yerevan, Refresh

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pachini, amemuahidi Kaibu Mkuu mpya wa OIF kuwa nchi yake na nchi wanachama watamuunga mkono kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Katika hotuba yake iliyodumu dakika chache, Louise Mushikiwabo amekiri kwamba ameipokea habari hiyo kwa "furaha nyingi", na "shukrani". Amesema akishukuru waliomteua kuchukuwa nafasi hiyo.

Kwa upande wa kushoto, katibu mkuu wa zamani wa Francophonie, Michaëlle Jean. Kwa upande wa kulia, Louise Mushikiwabo. Erevan, Oktoba 12, 2018.
Kwa upande wa kushoto, katibu mkuu wa zamani wa Francophonie, Michaëlle Jean. Kwa upande wa kulia, Louise Mushikiwabo. Erevan, Oktoba 12, 2018. LUDOVIC MARIN / AFP

"Nilikuja Erevan kwama Mnyarwanda kutoka Afrika, narudi kama mmoja kati ya viongozi wa Francophonie. Ninawakshukuru. "Familia hii ya Francophone ina uwezo mkubwa sana," amesema, akisifu taasisi hiyo kwa "sifa ya ufanisi na uwazi."

Lengo lake kama katibu mkuu atafanya kilio chini ya uwezo wake ili Jumuiya hii ya Francophonie "ipige hatua kubwa ulimwenguni". "Nilizunguka dunia kwa miezi miwili na nusu ili kukusanya mawazo na matarajio yenu. Jumuiya itaendelea na "wote", "wanachama wote", ameongeza Bi Mushikiwabo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.