Pata taarifa kuu
DRC-YUMBI-USALAMA

Uchunguzi: Mauaji ya watu 535 kutoka kabila la Banunu yalipangwa

Kwa mujibu wa uchunguzi ulionfayika katika mji wa Yumbi, nchini DRC, machafuko yaliojiri katika mji huo yaliosababisha watu 535 kutoka kabila la Banunu kupoteza maisha kwa kipindi cha siku mbili, yalipangwa. Umoja wa Mataifa unasema idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi.

Yumbi inapatikana katika Jimbo la Mai-Ndombe, DRC.
Yumbi inapatikana katika Jimbo la Mai-Ndombe, DRC. RFI
Matangazo ya kibiashara

Machafuko hayo yalioshuhudiwa wakati wa kampeni za uchaguzi mwezi Desemba mwaka jana yalizuka pale tu watu wa kabila la Banunu walipopanga kufanya shughuli za mazishi ya kiongozi wao katika ardhi inayo daiwa kuwa ya watu wa kabila la Batende.

Hata hivyo uchunguzi unaonyesha kuwa mauaji hayo yaliandaliwa, hasa kwamba kulikuwa na ujumbe uliotolewa kwa watu wa kabila la Banunu kuwatahadharisha na mauaji, lakini pia walioshambulia walitumia sio tu visu na mapanga lakini pia silaha za kivita.

Askofu wa kanisa Katoliki jijini Kinshasa Fridolin Ambongo ambae alizuru mji wa Yumbi amesema uchunguzi unahitajika ili kila mtu abebe mzigo wake.

Hata hivyo Gavana wa Jimbo la Mai-Ndombe, Gentini Gobila, ambae amekuwa akitajwa kuhusika na mauaji hayo, ametupilia mbali madai dhidi yake na kueleza kwamba hana sababu yoyote ya kuhusika na mauaji hayo.

Watu wa kabila la Batende wanalaumiwa kuhusika na mauaji hayo ambapo Gavana wa Jimbo la Mai-Ndombe, Gentini Gobila, ni kutoka kabila hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.