Pata taarifa kuu
NIGERIA-UCHAGUZI-SIASA

Matokeo ya uchaguzi wa urais kuanza kutangazwa Nigeria

Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria inatarajiwa kuanza kutangaza matokeo ya Uchaguzi wa urais uliowavutia wagombea 73, baada ya wapiga kura zaidi ya Milioni 72 kupiga kura Jumamosi iliyopita.

Maafisa wa Tume Ya Uchaguzi Nigeria (INEC) wakikusanya matokeo ya ya uchaguzi kutoka vituo vya kupigia kura tofauti Yola, katika Jimbo la Adamawa, Februari 24, 2019.
Maafisa wa Tume Ya Uchaguzi Nigeria (INEC) wakikusanya matokeo ya ya uchaguzi kutoka vituo vya kupigia kura tofauti Yola, katika Jimbo la Adamawa, Februari 24, 2019. © REUTERS/Nyancho NwaNri
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Mahmood Yakubu amesema matokeo hayo yataanza kutangazwa saa tano asubuhi saa za Nigeria, katika ukumbi wa Kimataifa jijini Abuja.

Raia wa Nigeria wanasubiri kwa hamu kufahamu ni nani atakayeshinda uchaguzi wa urais, huku ushindani ukitarajiwa kuwa kati ya rais Muhammadu Buhari na mpinzani wake wa karibu Atiku Abubakar.

Mmwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ameeleza kuwa zoezi la kutangaza matokeo hayo kutoka majimbo 36, yatafanyika kwa uwazi na yatatangazwa kutoka kila jimbo.

"Kila kitu kitafanyika katika ukumbi huu, tume ya kukusanya matokeo ambayo naongoza haipo sehemu nyingine katika jumba hili, kila kitu kipo hapa na matokeo yatakapowasili kila mmoja atafahamu ni nani ameingia na kazi ya tume itakuwa ni kuhakikisha kuwa inaweka mpangilio mzuri wa kupokea na kuwasilisha matokeo"

Wagombea 73 waliwania urais na ili kuibuka mshindi, ni sharti mgombea apate asilimia 25 ya kura zote zilizopigwa katika majimbo 24 kati ya 36.

Wakati huo huo, waangalizi wa Kimataifa wanatarajiwa kutoa ripoti ya awali kuhusu walichokiona wakati zoezi la kupiga kura likiendelea mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hata hivyo, Benson Olug buo, aliyeoongoza waangalizi wa ndani kutoka Shirika la Cleen Foundation, amesema, machafuko yaliyotokea katika baadhi ya majimbo lakini pia uchaguzi kucheleweshwa kuanza katika vituo kadhaa vya kupigia kura inashirishia umuhimu wa tume ya uchaguzi kufanyiwa marekebisho.

"Tunahitaji mageuzi ya mfumo wa uchaguzi, na tume ya Uchaguzi inastahili kuangaziwa upya, lakini pia tunahitaji kuja na adhabu kwa wale wanaosabisha machafuko wakati wa uchaguzi lakini pia tuangalie gharama ya kufanya uchaguzi kwa sababu ni ghali sana na inasababisha matatizo"

Kwa sasa wananchi nchini Nigeria, wanasubiri kufahamu ni nani atakuwa rais wao mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.