Pata taarifa kuu
GABON-SIASA-AFYA

Rais wa Gabon aruhusiwa kuondoka hospitali

Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba ameruhusiwa kuondoka hospitali ya kijeshi ya Rabat nchini Morocco ambako aliwasili mwishoni mwa mwezi Novemba. Kwa sasa Ali Bongo Ondimba ataendelea kupatiwa matibabu akiwa katika makazi binafsi katika mji mkuu wa Morocco, vyanzo kutoka washirika wa karibu wa rais Bongo vimesema.

Picha rasmi iliyotolewa na serikali ya Morocco ikimuonyesha Mfalme wa Morocco Mohammed VI (kushoto) na Rais wa Gabon Ali Bongo, katika hospitali ya kijeshi ya mji mkuu wa Morocco.
Picha rasmi iliyotolewa na serikali ya Morocco ikimuonyesha Mfalme wa Morocco Mohammed VI (kushoto) na Rais wa Gabon Ali Bongo, katika hospitali ya kijeshi ya mji mkuu wa Morocco. Handout / Moroccan Royal Palace / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kuondoka kwake ni uamuzi uliochukuliwa "baada ya idhini ya timu ya matibabu", kulingana na vyanzo hivyo.

Siku ya Jumatatu Ali Bongo alionekana hadharani kwa mara ya kwanza, akiwa na Mfalme wa nchi hiyo Mohammed VI aliyeenda kumtembelea.

Siku ya Jumatatu jioni viongozi wakuu nchini Gabon, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu na Makamu wa rais walifanya safari kwenda kumjulia hali rais wa nchi hiyo Ali Bongo Ondimba anaendelea kupatiwa matibabu katika mji mkuu wa Morocco, Rabat, kwa mujibu shirika la Habari la AFP likinukuu chanzo rasmi kutoka ikulu ya rais.

Makamu wa rais wa Gabon Pierre Claver Maganga, amewaambia raia wa nchi hiyo kuwa, rais Ali Bongo anaendelea vema na hivyo hakuna ya kuwa na wasiwasi.

Ugonjwa unaosumbua, haujawekwa wazi lakini, inaaminika kuwa alipata kiharusi mwishoni mwa mwezi Oktoba, wakati alipokuwa amekwenda nchini Saudi Arabia kuhudhuria mkutano wa kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.