Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Ripoti ya GEC: CENI na Mahakama ya Katiba viko mikononi mwa ofisi ya rais DRC

Ripoti kutoka Shirika linalotafiti kuhusu nchini ya DRC kutoka chuo Kikuu cha New York nchini Marekani GEC, ineleza kuwa Ofisi ya rais ina ushawishi mkubwa kwa Tume ya Uchaguzi CENI, na Mahakama ya Katiba kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwezi ujao.

Rais wa DRc Joseph Kabila.
Rais wa DRc Joseph Kabila. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Utafiti wa Shirika hilo unanesha kuwa, uongozi wa CENI na Mahakama ya Katiba, hauwezi kukataa maagizo kutoka kwa ofisi ya rais Joseph Kabila.

GEC inaonya kuwa, hali hii huenda ikaathiri Uchaguzi huo ambao Tume imekuwa ikisema kuwa utakuwa huru na haki.

"Tuhuma hizi za kutumiwa kwa mchakato wa kisiasa, ukosefu wa makubaliano kwa wanasiasa na mvutano ambao unaweza kutokea vinaweza kusababisha DRC kukumbwa tena na machafuko mapya," wanasema wataalam katika ripoti hii, yenye kichwa cha habari, "DRC : uchaguzi wa hatari zote ".

"Tuhuma zote hizi zisizokuwa na msingi zinalenga kuandalia nafasi wale ambao wanataka kususia uchaguzi. Kuna hatua zinazofanyika ili kuzuia uchaguzi usifanyike," amejibu Jean-Pierre Kambila, naibu mkurugenzi katika ofisi ya Rais Kabila.

Uchaguzi Mkuu wa Desemba 23, 2018 utapelekea anapatikana mrithi wa Rais Joseph Kabila. Uchaguzi huu tayari umeahirishwa mara mbili mwaka 2016 na mwaka 2017.

Rais Kabila, ambaye hatowania tena baada ya kuhudumu mihula miwili, alimteua Waziri wake wa zamani wa Mambo ya Ndani Emmanuel Ramazani Shadary kama mtu atakayepeperusha bendera ya chama cha PPRD katika uchaguzi huo wa urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.