Pata taarifa kuu
BURUNDI-DEMOKRASIA

Burundi yaadhimisha miaka 25 tangu kutokea mauaji ya Melchior Ndadaye

Burundi hii leo inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 tangu kutokea kwa mauji ya hayati Melkior Ndadaye, kinara wa demokrasia nchini humo. Siku hii inakuja wakati nchi hii inaendelea kukumbwa na mvutano wa kisiasa, huku usalama ukiendelea kuhatarishwa.

Melchior Ndadaye, rais wa kwanza wa Burundi kutoka jamii ya Wahutu aliyechaguliwa chini ya misingi ya kidemokrasia mnamo mwaka 1993.
Melchior Ndadaye, rais wa kwanza wa Burundi kutoka jamii ya Wahutu aliyechaguliwa chini ya misingi ya kidemokrasia mnamo mwaka 1993. © AFP/DABROWSKI
Matangazo ya kibiashara

Melchior Ndadaye rais wa kwanza, kutoka jamii ya Wahutu, aliyechaguliwa katika misingi ya kidemokrasia aliauawa usiku wa Octoba 21 mwaka 2003 na kundi la wanajeshi wa kutoka jamii ya Watutsi wenye msimamo mkali ambao walishindwa kuvumilia kuona mtu kutoka jamii ya Wahutu akiongoza nchi hiyo, iliyotawaliwa na Watutsi kwa miaka zadi ya 31.

Melchior Ndadaye aliibuka mshindi kwenye uchaguzi wa mwezi Julai mwaka 2003 dhidi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo,Pierre Buyoya chini ya chama chake cha SAHWANYA -FRODEBU. Ndadaye hakupata muda wa kuongoza nchi hiyo kwani miezi mitatu tu baadaye aliuawa, na hivyo kuzuka machafuko ya kikabila nchini humo, yaliosababisha watu zaidi ya laki nane kupoteza maisha huku wengine wakiitoroka nchi hiyo.

Mkataba wa wa amani na maridhiano uliosainiwa jijini Arusha, ndio uliowaleta pamoja kwa mara ya tena Warundi.

Mwaka 2005, Bunge la taifa hilo, lilipasisha sheria inayo mkubali Melchior Ndadaye kama kinara wa demokrasia nchini Burundi.

Kiongozi wa sasa wa chama hicho cha hayati Melchior Ndadaye, bwana Leonce Ngendakumana amesema anasikitika kuona misingi walioachiwa na kinara huyo ambayo ni udumishwaji wa demokrasia amani na utulivu nchini vimekuwa vikipuuziwa.

Kama ilivyokuwa ada, viongozi mbalimbali wa serikali ya Burundi kwa sasa wanawahudhuria misa ya kumuombea kiongozi huyo kwenye kanisa la Cathedrale Regina Mundi jijini Bujumbura na sherehe zingine zitaendelea kwenye eneo alipozikwa katika manispaa ya jiji la Bujumbura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.