Pata taarifa kuu
DRC-AFYA-WHO

Watu watatu waliokuwa wameambukizwa Ebola, wapona Butembo

Matumaini yameanza kushuhudiwa mjini Butembo Mashariki mwa DRC baada ya watu watatu waliokuwa wameambuzwa Ebola kupona kabisa.

Maafisa wa afya wakipambana na Ebola
Maafisa wa afya wakipambana na Ebola Photo: Florence Morice / RFI
Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa wagonjwa waliopona ni Arlette.

“ Kweli nimepona nimetuzwa vizuri , ugonjwa wa Ebola upo na wanaopata huduma ya haraka wanapona,” alisema Arlette akionekana kuwa mwenye furaha kubwa.

Madaktari wanasema wale wanaombukizwa ugonjwa huu, wakimbilie katika huduma za matibabu.

“Tuelewe kwamba kuna ugonjwa wa Ebola na watu walioambukizwa wanastahili kupata matibabu, kupona kwao ndio furaha yetu ” amesema Daktari Justice Iyomleto.

Gavana wa Jimbo la Kivu Kaskazini Julien Kahongya amesema, yeyote asikubali kudanganywa kuwa ugonjwa huo haupo.

“Tunajaribu sana kuumaliza ugonjwa huu, lakini mtu asije kuwaambia kuwa hakuna Ebola huyo ni muuaji, alisema kwa msisitizo Gavana Kahongya.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha ni idadi ya watu waliipoteza maisha imefikia 109 kati ya watu 179 walioambukizwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.