Pata taarifa kuu
MALI-UNSC-USALAMA

UN kuwachukulia hatua kali watu wanaovunja mkataba wa amani Mali

Baraza la Usalama la Umoja wa Matiafa limetishia kuwachukulia hatua kali hasa vikwazo watu wanahusika katika kuhatarisha usalama na amani nchini Mali.

Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York, Agosti 29, 2018.
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York, Agosti 29, 2018. © REUTERS/Andrew Kelly
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza kwa mwaka mmoja mlolongo wa vikwazo dhidi ya Mali, na kutishia kuchukua vikwazo kila mmoja dhidi ya viongozi wa makundi ya waasi wanaotuhumiwa kukiuka mkataba wa amani wa mwaka 2015.

Azimio la kuongeza mlolongo wa vikwazo hivyo lilipitishwa kwa kauli moja Alhamisi wiki hii na wajumbe 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Nchini Mali, "mafanikio yaliyopatikana bado hayatoshi" na "muda wa kutoa onyo umemalizika," alisema Naibu Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, Anne Gueguen. "Tunahitaji kuona maendeleo kutoka pande zote," mwenzake wa Uingereza Jonathan Allen aliwaambia waandishi wa habari.

Akitoa mfano wa "viongozi kutoka makundi ya waasi ambao wanakiuka mkataba wa amani kutokana na uhusiano wao na makundi ya wahalifu," Anne Gueguen aliongeza kuwa Ufaransa imekua ikipendekeza "vikwazo viweze kuchukuliwa".

Msimamo wa Urusi na China kuhusu vikwazo vya kila mmoja kwa viongozi wa makundi ya waasi bado haujawekwa wazi. Nchi hizi mbili mwaka mmoja uliopita zilijizuia wakati kulianzishwa mpango wa vikwazo dhidi ya Mali, mpango ambao ulipendekezwa na Ufaransa.

Katika ripoti ya tarehe 8 Agosti, wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mali walishtumu viongozi wa makundi waliotia saini mkataba wa amani wa mwaka 2015, ikiwa ni pamoja na Alkassoum Ag Abdoulaye, Mkuu wa majeshi ya waasi wa kundi la CPA, kundi ambalo linashtumiwa kuendesha mashambulizi mawili dhidi ya majeshi ya Mali mnamo mwaka 2017 na 2018. Ripoti hiyo pia imemtaja kiongozi mwingine wa CPA, Mohamed Ousmane Ag Mohamedoune, pia anayetuhumiwa kukiuka mkataba amani.

Wataalam pia wanashtumu " visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya raia ambavyo vinaendeshwa na vikosi vya usalama wakati wa oparesheni dhidi ya magaidi." Serikali ya Mali ilikiri kutokea kwa visa hivyo.

Hata hivyo baadhi ya makundi ya waasi yamekosoa ripoti hiyo na kusema kuwa ni uzushi mtupu kwa lengo la kuwapaka matope.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.