Pata taarifa kuu
MALI-UCHAGUZI-SIASA

Matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais kutangazwa Mali

Tume ya Uchaguzi nchini Mali inatarajia kutangaza matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi Alhamisi hii, Agosti 16. Matokeo hayo yatatangzwa kwenye makao makuu ya Wizara ya Utawala ya Mali.

Askari wakitoa ulinzi mbele ya Wizara ya Utawala ya Mali huko Bamako Agosti 2, 2018.
Askari wakitoa ulinzi mbele ya Wizara ya Utawala ya Mali huko Bamako Agosti 2, 2018. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Kama hakutakua na mabadiliko yoyote katika dakika ya mwisho, matokeo ya awali ya duru ya pili ya uchaguzi yatatangazwa Alhamisi hii, na tayari ripoti za uchguzi huo zilizokua zikisubiriwa kutoka maeneo matatu ya mwisho zimewasilishwa kwenye Tume ya Uchaguzi huko Bamako.

Kwa mujibu wa duru rasmi, Waziri wa Utawala wa Mali, Mohamed Ag Erlaf ndiye anatarajiwa kutangaza jina la mshindi wa uchaguzi huo, mgombea aliyeshindwa, kiwango cha ushiriki, na takwimu nyingine kutoka kwa shughuli ya Tume ya Kitaifa ya kukusanya Matokeo ya uchaguzi.

Tayari mwakilishi wa mgombea urais kutoka kambi ya upinzani Soumaïla Cissé amejiondoa kwenye kamati hiyo akipinga "matokeo ya uchaguzi". Kauli kama hiyo ilitolewa siku ya Jumatano, Agosti 15 jioni mbele ya vyombo vya habari na muungano unaounga mkono mgombea Soumaïla Cissé.

Jumuiya ya kimataifa inafuatilia kwa karibu hali hiyo nchini Mali. Wawakilishi wake wakuu huko Bamako, ujumbe wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, ECOWAS, wametoa taarifa ambapo wametaja kuwa mchakato wa "baada ya uchaguzi ulikua wa utulivu na uliheshimiwa na pande zote katika uchaguzi".

"Pande zote ikiwa ni kambi ya rais anayemaliza muda wake au kambi ya upinzani, wote wanasema kuwa wameshinda uchaguzi, lakini sio kweli, hakutakuwa na washindi wawili! Hiyo ni maneno ya kisiasa. Tunapaswa kuwa watulivu na kusubiri matokeo, " wamesema baadhi ya raia wa Mali wakihojiwa na mwandishi wetu Coralie Perret.

Taarifa hiyo imewataka wagombea Ibrahim Boubacar Keïta na Soumaïla Cissé, pamoja na wafuasi wao kutumia njia za kisheria na za kikatiba ili kutatua migogoro hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.