Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Uchaguzi DRC: Orodha ya vyama vya siasa vilivyoruhusiwa yazua utata

Orodha ya vyama 599 na miungano 77 ya vyama vya kisiasa vilivyoruhusiwa kufanya shughuli zao nchini DRC, na ambavyo vitaweza kushiriki katika uchaguzi wa mwezi Desemba 2018 imechapishwa kwenye Jarida la serikali. Tayari orodha hiyo imepingwa na baadhi ya vyama vya siasa na mashirika ya kiraia.

Makao makuu ya Bunge, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Makao makuu ya Bunge, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wikimédia
Matangazo ya kibiashara

Kwa mfano kwenye orodha hiyo, kuna vyama vinne vya kisiasaambavyo vina jina la chama cha UDPS, chama kikuu cha upinzani nchini DRC. Baadhi ya mashirika ya kiraia kama Acaj yamesema orodha hiyo haikubailiki, huku yakisema kuwa orodha hiyo inaweza kuzua vurugu wakati wa kipindi cha uchaguzi.

 

Shirika la Acaj linabainisha kwa mfano kwamba vyama vinne vya kisiasa vina jina moja "UDPS", huku viwili vikiwa na makau makuu moja namba moja ya usajili. Vyama hivi ni pamoja na UDPS inayoongozwa na Waziri Mkuu Bruno Tshibala na UDPS inayoongozwa na Felix Tshisekedi.

Kwa upande wa Georges Kapiamba, mratibu wa Acaj, hali hii imewekwa kwa makusudi na serikali kwa lengo la kudhoofisha upinzani: "Hii itazua mkanganyiko kwa wapiga kura na hili ndilo wanalotaka wale ambao wamechukua uamuzi huu kuhusiana na vyama vya upinzani. Ni dhahiri kuwa kunaweza kutokea vurugu kati ya wanachama wa makundi mbalimbali ya upinzani. "

Kwa mujibu wa Kapiamba, ni mbinu ya vyama vinavyounga mkono serikali na utawala ili kuzuia vyama vya upinzani kufikia idadi ya kiutosha ya wabunge katika uchaguzi wa wabunge ujao kwa kupitisha maamuzi bila upinzani wowote: "Inatakiwa kuvunja upinzani ili kupunguza bahati ya kuwa na wafuasi wengi katika nchi hii. Vyama vinavyounga mkono serikali na utawala ndivyo vitanufaika na hali hii, " ameongeza Georges Kapiamba

Vyama hivyo ambavyo vinaona kuwa vimefanyiwa unyonge bado vina nafasi ya kukata rufaa, lakini George Kapiamba ameshauri kutotumia njia ya mahakama na kupendekeza shinikizo la moja kwa moja kwa wizara ya mambo ya ndani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.