Pata taarifa kuu
MAY DAY-KAZI

Shirika la Kazi duniani latoa ripoti kuhusu ajira duniani

Shirika la Kazi duniani ILO linasema katika ripoti yake kuwa, watu Bilioni 2, sawa na asilimia 61 ya watu walioajiriwa, wapo katika ajira zisizo rasmi. 

Wafanyakazi wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya wafanyakazi  Mei 1, 2017, huko Lyon, katikati mashariki mwa Ufaransa.
Wafanyakazi wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya wafanyakazi Mei 1, 2017, huko Lyon, katikati mashariki mwa Ufaransa. JEFF PACHOUD / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya ILO inaeleza pia kuwa, watu hao wanatoka katika mataifa yanayoendelea kiuchumi, huku wanawake wakiwa ni Milioni 740.

Barani Afrika, asilimia 85.8 ya ajira sio rasmi huku Asia ikiwa katika nafasi ya pili kwa silimi 68.2.

Aidha, ripoti hii iliyotolewa wakati dunia inaadhimisha sikukuu ya wafayakazi, inaeleza pia kuwa idadi kubwa ya watu wanaojihusisha katika ajira hizo sizozo rasmi ni wanaume, huku wanawake wakiwa ni asilimia 58.1.

Inaelezwa kuwa, kazi nyingi zilizo rasmi zinafanywa na watu wanaoishi katika maeneo ya vijijini.

Pamoja na hilo ukosefu wa elimu kwa watu wengi pia inachangiwa pakubwa kutokana na hali hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.