Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Ethiopia: Serikali yakashifiwa kuwakamata tena wanahabari na wanasiasa wa upinzani

Wanaharakati wa haki za binadamu na wae wa vyombo vya habari wameikashifu vikali Serikali ya Ethiopia baada ya kuwakamata kwa mara nyingine waandishi wa habari na wanasiasa wa upinzani ambao waliachiwa majuma kadhaa yaliyopita.

Maandamano jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kupinga hali ya hatari nchini humo.
Maandamano jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kupinga hali ya hatari nchini humo. PHOTO | AFP
Matangazo ya kibiashara

Andualem Aragie kiongozi wa chama cha upinzani cha UDJ, mwanahabari Eskinder Nega na Temesgen Desalegn, mwandishi wa blogu Befeqadu Hailu na Zelalem Workagegnehu walikamatwa mwishoni mwa juma wakati wa sherehe za kupongeza kuachiwa kwao.

Nchi ya Ethiopia tayari imewaachia huru wafungwa zaidi ya 6000 tangu mwezi Januari wakiwemo waandishi wa habari maarufu na wanasiasa wa upinzani.

Aliyekuwa waziri mkuu Hailemariam Desalegn kabla ya kujiuzulu kwake alisema kuwaachia huru wafungwa hao wa kisiasa ni katika kuonesha nia ya kutafuta maridhiano ya kitaifa kutokana na mfululizo wa maandamano yaliyoanza mwaka 2015.

Licha ya kujiuzulu kwa Desalegn bado hali ya hatari imeendelea kutekelezwa nchini humo licha ya maandamano ya upinzani wa jamii ya Oromiya na Amhara.

Amha Makonnen ambaye aliwatetea wanasiasa na waandishi hao wa habari, amesema wateja wake walikamatwa kwa kukiuka makataa ya hali ya hatari na pia kwa kuonesha bendera zilizopigwa marufuku.

Chini ya hali ya hatari iliyotangazwa nchini Ethiopia mwaka huu, watu wanakatazwa kufanya mikusanyiko wakati wa muda wa makataa hiyo bila kupata idhini maalumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.