Pata taarifa kuu
MALI-UGAIDI-WANAJESHI

Wanajeshi wanne wa Mali wauawa baada ya gari kukanyaga bomu

Wanajeshi wanne wa Mali wameuawa baada ya gari walimokuwa wanasafiria kukanyaga bomu iliyokuwa imetegwa ardhini katika mji wa Dialloube katikati ya nchi hiyo.

Magari ya kijeshi nchini Mali
Magari ya kijeshi nchini Mali Pascal Guyot, AFP
Matangazo ya kibiashara

Jeshi nchini humo limethibitisha kutoka kwa tukio hilo wakati maafisa wake walipokuwa njia kurejea kambini baada ya makabiliano na makundi ya kijihadi.

Serikali ya Mali inasema, operesheni hiyo ilizaa matunda baada ya magaidi 10 kuuawa na wengine kujeruhiwa.

Wiki iliyopita, wanajeshi wengine wa Umoja wa Mataifa walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika mazingira kama haya walipokuwa ndani ya gari yao.

Makundi ya kigaidi yanayoshirikiana na Al Qeada yameendelea kuisumbua serikali ya Mali hasa eneo la Kaskazini tangu mwaka 2012.

Jeshi la Ufaransa lilikuja nchini humomwaka 2013 kuisadia Mali kumenyana na magaidi hao.

Waziri Mkuu Boubeye Maiga amesema operesheni za kijeshi dhidi ya makundi hayo ya kigaidi zinazaa matunda.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.