Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALI-USALAMA

Mateka wa Ufaransa Mali: Familia yaitaka serikali ya Ufaransa kuchukua hatua

Mwaka mmoja tangu kutekwa kwa Sophie Pétronin, raia wa Ufaransa kaskazini mwa Mali katika mji wa Gao Desemba 24 mwaka 2016, familia na watu wake wa karibu wamekusanyika ili kuishinikiza serikali ya Ufaransa kufanya jitihada za kuachiwa kwake.

Askari wa Minusma wakiwasikiliza wakazi wa mkoa wa Gao kaskazini mwa Mali.
Askari wa Minusma wakiwasikiliza wakazi wa mkoa wa Gao kaskazini mwa Mali. MINUSMA/Harandane Dicko
Matangazo ya kibiashara

Tangu kutekwa kwa mwanamama huyo aliekuwa akiwahudhumia watoto mayatima kaskazini mwa Mali, ambae alionekana mara moja mwezi Julai kupitia mkanda wa video na kundi la muungano wa wa makundi ya kijihadi katika ukanda wa Sahel.

Arnaud Granouillac, mwipwa wa Sophie Pétronin ambae anashirikiana na watu wengine zaidi ya mia nne wanaounga mkono familia, ameitaka serikali ya Ufaransa kushughulikia kwa vitendo swala hili la kuachiwa kwa mwanamama huyo.

Sophie Pétronin alikuwa anaongoza shirika linalo washughulikia watoto yatima katika mji wa Gao kaskazini mwa Mali kabla ya kutekwa na kundi la wapiganahi wa kijihadi.

Watu kadhaa waliuawa nawengine wanaendelea kushikiliwa na makundi ya wanamgambo wa kiislamu katika maeneo kadhaa ya nchi ya Mali hasa katika mji wa Gao ambapo inaaminika kwamba ni ngome kubwa ya makundi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.