Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA-AFRIKA

Mugabe: Kiongozi wa mwisho barani Afrika kupigania uhuru wa nchi yake

Robert Mugabe aliyejiuzulu kama rais wa Zimbabwe siku ya Jumanne, alikuwa kiongozi wa mwisho barani Afrika aliyeingia madarakani baada ya kuongoza nchi yake kupata uhuru mwaka 1980.

Robert Mugabe
Robert Mugabe 路透社
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa Mugabe mwenye umri wa miaka 93, aliyeongoza Zimbabwe kwa muda wa miaka 37, aliamua kuondoka baada ya shinikizo ndani ya chama chake na raia wa nchi hiyo.

Yote haya yalikuja baada ya jeshi kuamua kuingilia kati mzozo wa kisiasa nchini humo hasa ndani ya chama tawala ZANU PF.

Mbali na Mugabe, hawa ni baadhi ya waasi waliongoza nchi zao baada ya uhuru.

Kwame Nkrumah, Ghana -

Alizaliwa mwaka 1909.

Baada ya nchi yake kupata uhuru mwaka 1957, alikuwa Waziri Mkuu na baadaye kuwa rais baada ya nchi yake kubadilishwa jina na kuitwa Ghana kutoka Gold Coast.

Mwaka 1966 aliondolewa madarakani baada ya kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi na kukimbilia nchini Romania mwaka 1972, alikofia.

Ahmed Sekou Toure, Guinea -

Aliongoza nchi ya Guinea, tangu uhuru mwaka 1958 hadi kifo chake mwaka 1984.

Ni kiongozi aliyepinga ushawishi kutoka kwa wakoloni Ufaransa chini ya kiongozi wa wakati huo Jenerali Charles de Gaulle.

Leopold Sedar Senghor, Senegal -

Aliongoza Senegal baada ya Uhuru mwaka 1960 na kusalia madarakani kwa muda wa miaka 20 kabla ya kukimbilia nchini Ufaransa alikofia mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 95.

Felix Houphouet-Boigny, Ivory Coast -

Aliongoza nchi yake tangu uhuru mwaka 1963, hadi kifo chake mwaka 1993.

Atakumbukwa sana kwa kupigania uhuru na kuhimiza waafrika kujitegemea.

Julius Nyerere, Tanzania -

Alikuwa muasisi wa chama cha TANU mwaka 1954, kilichosaidia upakanaji wa uhuru wa nchi yake mwaka 1964.

Aliongoza nchi hiyo tangu mwaka 1961 hadi 1985 na baadaye kujiuzulu.

Jomo Kenyatta, Kenya -

Alikuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wa nchi yake na hata kufungwa jela na wakoloni kutoka Uingereza.

Aliongoza Kenya, tangu mwaka wa uhuru 1963 hadi kifo chake 1978.

Mtoto wake Uhuru Kenyatta ndio rais wa sasa wa nchi hiyo. Uchaguzi wake umeendelea kuzua maswali iwapo una uhalali.

Kenneth Kaunda, Zambia -

Rais wa kwanza wa nchi yake iliyopata uhuru mwaka 1964. Anakumbukwa kupigania uhuru kutumia njia ya amani.

Aliongoza nchi yake kwa muda wa miaka 27 tangu uhuru.

Mwaka 1991, alishindwa wakati wa Uchaguzi Mkuu na kukubali matokeo.

Kamuzu Banda, Malawi -

Alikuwa Waziri Mkuu wa nchi yake kwa zaidi ya miaka 30, baada ya uhuru mwaka 1966.

Mwaka 1993, baada ya kupata shinikizo ndani na nje ya nchi yake, alikubali kufanyika kwa kura ya maoni ili kuwepo kwa vyama vingi.

Hakuchaguliwa tena wakati wa Uchaguzi wa mwaka 1994, miaka mitatu baadaye alifariki dunia akiwa nchini Afrika Kusini.

Samora Machel, Msumbiji -

Alipambana na wakoloni wa Kireno kupitia chama chake cha Frelimo.

Baada ya uhuru mwaka 1975, alikuwa rais wa kwanza wa nchi hiyo hadi kuuawa kwake mwaka 1986, alipopata ajali ya ndege nchini Afrika Kusini.

Mkewe, Graca, aliolewa na rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela mwaka 1998.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.