Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-AJALI

Watu watatu wafariki katika ajali ya ndege ya mizigo Cote d'Ivoire

Ndege moja ya mizig, iliyokua ikibeba mizigo ya jeshi la Ufaransa, kulingana na vyombo vya habari vya Cote d'Ivoire, imeanguka katika bahari ya nchini hiyo , muda mfupi baada ya kuondoka mji mkuu wa Abidjan.

Kikosi cha wapiga mbizi wakitafuta kwenye eneo la ajali ya ndege aina ya Turboprop ATR-72, aktika eneo la Laos, karibu na Pakse, Oktoba 18, 2013.
Kikosi cha wapiga mbizi wakitafuta kwenye eneo la ajali ya ndege aina ya Turboprop ATR-72, aktika eneo la Laos, karibu na Pakse, Oktoba 18, 2013. REUTERS/Chaiwat Subprasom
Matangazo ya kibiashara

Inasemekana kwamba watu watatu wamefariki na wengine wamejeruhiwa.

Inaarifiwa kuwa kuna watu ambao walinusurika katika ajali hiyo. Mashahidi wanasema mabaki ya ndege hiyo aina ya Turboprop yalisombwa hadi katika ufukwe.

Maafisa wa usalama nchini Cote d'Ivoire wanasema ndege hiyo ilianguka wakati wa mvua kubwa karibu na bandari ya Bouet.

Baadhi ya mashahidi wakinukuliwa na shirika la habari la Reuters wanasema watu wanne walipotez maisha, huku wakibaini kwamba miili miwili ilitolewa kutoka kwa ndege hiyo huku mingine miwili ikionekana katika mabaki ya ndege.

Kwa mujibu wa maafisa wa usalama wa Cote d'Ivoire ndege hiyo aina ya Turboprop imedaiwa kutengezwa nchini Ukrain.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.