Pata taarifa kuu
NIGERIA-UN-USALAMA

Zannah Mustapha atunukiwa tuzo na tume ya Umoja wa Mataifa

Wakili raia wa Nigeria aliyesaidia kufanikisha kuachiliwa huru kwa wasichana 100 wa Chibok waliokuwa wametekwa na Boko Haram, amepata Tuzo kutoka kwa Umoja wa Mataifa.

Kundi la wanafnzi wasichana 8 2wa Chibok walioachiliwa na Boko Haram Mei 6, 2017.
Kundi la wanafnzi wasichana 8 2wa Chibok walioachiliwa na Boko Haram Mei 6, 2017. REUTERS/Zanah Mustapha
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi imesema wakili huyo Zannah Mustapha amepata tuzo ya kila mwaka ya Nansen kutokana na jitihada zake kuwasaidia wasichana hao.

Wakili huyo mwenye umri wa miaka 50, amesema amefurahi sana kupokea tuzo hiyo na hakutarajia kuwa angeteuliwa.

Aidha, amesema kuwa ataendelea kufanya bidii na kutumia uwezo wake kusaidia kuwaachiliwa huru kwa mamia ya wasichana wengine ambao bado wako mikononi mwa Boko Haram.

Mustafa ambaye pia alianzisha shule kuwasaidia watoto Kaskazini kupata elimu mwaka 2010, anafahamika sana Kaskazini mwa Nigeria baada ya kuwa wakili wa familia ya Mohammed Yusuf, mwanzilishi wa Boko Haram aliyefia jela mwaka 2009.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.