Pata taarifa kuu
NIGERIA-CAMEROON-BOKO HARAM-USALAMA

Amnesty International: Boko Haram yaua watu 400 tangu mwezi Aprili

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Amnesty International linasema kuwa kundi la Boko Haram limewauwa watu 400 tangu mwezi Aprili mwaka huu.

Jiji la Maiduguri na viunga vyake, kaskazini mashariki mwa Nigeriaumekua ukilengwa na mashambulizi ya Boko Haram (hapa ni baada ya shambulio la Machi 15 2017).
Jiji la Maiduguri na viunga vyake, kaskazini mashariki mwa Nigeriaumekua ukilengwa na mashambulizi ya Boko Haram (hapa ni baada ya shambulio la Machi 15 2017). STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Amnesty International inasema mauaji mengi yametekelezwa nchini Nigeria na Cameroon, na idadi hii ni mara mbili ikilinganishwa na miezi mitano iliyopita.

Ripoti ya Shirika hilo inaeleza kuwa, wasichana wadogo walitumiwa na kundi hilo kutekeleza mauaji hayo kwa kujilipua baada ya kufungwa mabomu mwilini.

Mauaji haya yameelezwa na Amnesty International kama ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na vita vya uhalifu.

Tangu kuanza kutekeleza mashambulizi mwaka 2009, raia watu 20,000 wameuawa nchini Nigeria na nchi jirani huku wengine Milioni 2.6 wakiyakimbia makwao.

Amnesty International inataka Jumuiya ya Kimataifa kufanya zaidi kushinda kundi hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.