Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-MUGABE-HAKI

Kinga iliyotolewa kwa Grace Mugabe kufutiliwa mbali mahakamani

Nchini Afrika Kusini, mwanamke anayemshutumu mkewe rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kumshambulia, amemefungua mashitaka mbele ya mahakama ya Afrika Kusini ili kutaka kinga iliyotolewa kwa Grace Mugabe ifutiliwe mbali.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (kushoto) na mkewe Grace Mugabe (kulia).
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (kushoto) na mkewe Grace Mugabe (kulia). ( Photo : Alexander Joe /AFP )
Matangazo ya kibiashara

"Tuliwasilisha maombi yetu siku ya Jumatano mbele ya Mahakama Kuu ya Pretoria ili Grace Mugabe aondolewe kinga aliopewa, " amesema Bi Engels.

Waziri alitafsiri vibaya sheria hiyo kwa kumpa kinga muhalifu. Alitumia kanuni isizofaa kwa kutoa kinga hiyo, "alisema Willie Spies, mwanasheria wa Gabriella Engels.

Gabriella Engels, mwanamitindo wa miaka 20, aliwasilisha kesi ya kushambuliwa dhidi ya mkewe wa Rais Robert Mugabe.

Serikali ya Afrika Kusini badala yake ilijitetea na kusema ilichukua hatua hiyo kwa sababu Bi.Mugabe ana kinga ya kidiplomasia na hivyo asingeweza kupelekwa Mahakamani.

Gabriella Engels ameendelea kusisitiza kuwa alivamiwa na kifaa cha umeme jijini Johannesburg katika hoteli ambayo Bi.Mugabe na wanawe wawili wa kiume walikuwa wanaishi.

Engels anaitaka Mahakama kubadilisha kinga ya kidiplomasia aliyopewa Bi.Mugabe na kumsadia kurudi nyumbani na kuweka wazi kuwa haizuii kushtakiwa kwake Mahakamani.

Kesi hiyo imeratibiwa kusikilizwa tarehe 19 mwezi Septemba.

Wanaharakati na wanasiasa wa upinzani pia wamelaani hatua ya serikali ya Afrika Kusini kumruhusu Bi.Mugabe kuondoka nchini humo.

Mwanamitindo Gabriella Engels wakati wa mkutano na waandishi wa habari akitoa maelezo jinsi alivyo shambuliwa na Grace Mugabe.
Mwanamitindo Gabriella Engels wakati wa mkutano na waandishi wa habari akitoa maelezo jinsi alivyo shambuliwa na Grace Mugabe. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.