Pata taarifa kuu
NIGERIA

Kikao cha Baraza la Mawaziri nchini Nigeria cha ahirishwa

Kikao cha Baraza la Mawaziri nchini Nigeria ambacho hufanyika kila wiki, kimeahirishwa hata baada ya rais Muhammadu Buhari kurejea nyumbani baada ya miezi mitatu nchini Uingereza alikokuwa anapata matibabu.

Rais wa Nigeria  Mohammadu Buhari
Rais wa Nigeria Mohammadu Buhari Sunday AGHAEZE / NIGERIA STATE HOUSE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Haijaelezwa sababu ya kuahirishwa kwa kikao hicho, lakini tangu kurejea kwake nyumbani, amekuwa akifanya kazi akiwa nyumbani kwake.

Hatua hii imekuja baada ya kuripotiwa kuwa, panya aliharibu vifaa vyake vya kazi kama makaratasi, viti na meza katika Ikulu ya Abuja.

Msemaji wake Garba Shehu amesema Ofisi ya rais Buhari inahitaji ukarabati kabla ya kiongozi huyo kurejea kazini.

Buhari amerejea kazini wakati huu baadhi ya raia wa Nigeria wakiendelea kushinikiza kujiuzulu kwake, kwa madai kuwa ameshindwa kuongoza kwa sababu ya afya yake.

Kumekuwa na maaandamano ya wiki kadhaa kushinikiza hili lakini rais Buhari amesema sasa anaendelea vizuri na yuko tayari kuendelea na kazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.