Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Muhammadu Buhari: Naendelea vizuri

Kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miezi mitatu, rais wa Nigeria Muhammadu Buhari aliwahutubia wananchi wake akiwa nchini mwake, Nigeria.

Muhammadu Buhari, rais wa Nigeria, alirudi nchini mwake Agosti 19, 2017, baada ya miezi mitano mjini London kwa sababu ya matibabu.
Muhammadu Buhari, rais wa Nigeria, alirudi nchini mwake Agosti 19, 2017, baada ya miezi mitano mjini London kwa sababu ya matibabu. Nigeria Presidency/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake kwa taifa iliyorushwa kwenye televisheni ya taifa, rais Buharii aliwashukuru Wanigeria kwa "sala" zao, huku akitoa wito wa umoja na alionyesha dhamira yake ya kupambana dhidi ya ugaidi. Hakuzungumzia kuhusu hali yake ya afya.

Rais Buhari alitoa hotuba fupi. Hotuba yake ilidumu dakika 3 na sekunde 30. Rais wa Nigeria alionekana mdhaifu.

Kwa hotuba yake hii kwanza kwa Wanigeria tangu kurudi kutoka London baada ya siku mia ya kutokuwepo nchini, siku ya Jumamosi, Agosti 19, Muhammadu Buhari alipendekeza kutoa hotuba kwa kiwango cha uwezo wake wa sasa wa kimwili.

Pia aliwashukuru Wanigeria kwa maombi yao na hajasikika akizungumzia hali yake ya afya.

Usalama wapewa kipaumbele

Hotuba ilikua fupi, na iligubikwa na masuala ya usalama. Rais wa Nigeria alithibitisha "tamko la vita dhidi ya uhalifu na ugaidi". Pia alithibitisha nia yake ya kuangamiza kundi la Boko Haram.

Muhammadu Buhari hakuzungumzia kuhusu kugawana majukumu kati yake na makamu wa rais. Na haijulikani kama ataendelea kutekeleza majukumu yake kikamilifu kama inavyomruhusu Katiba ya Nigeria, au atakabidhi baadhi ya madaraka yake kwa makamu wake, Yemi Osinbajo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.