Pata taarifa kuu
NIGERIA

Rais Buhari arejea nyumbani baada ya siku zaidi ya 100 London

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, jana Jumamosi amerejea nyumbani akitokea London Uingereza alikokuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miezi mitatu.

Rais Muhammadu Buhari na makamu wake Yemi Osinbajo  katika uwanja wa ndege wa Abuja, 19 08  2017.
Rais Muhammadu Buhari na makamu wake Yemi Osinbajo katika uwanja wa ndege wa Abuja, 19 08 2017. Présidence nigériane
Matangazo ya kibiashara

Buhari amepokelewa na Wafuasi wake waliojipanga katika barabara za mji mkuu wakiimba na kucheza, ambapo maafisa wa ngazi za juu serikalini akiwemo makamu wake nao walikusanyika kumkaribisha Buhari.

Buhari mwenye umri wa miaka 74 aliondoka nchini mwake mnamo Mei 7 ambapo kutokurejea kwake kwa muda mrefu kulisababisha mvutano ambapo wananchi waliandamana na kutoa wito kumtaka arejee nyumbani au ajiuzulu.

Taarifa ya ikulu imeeleza kuwa rais Buhari, atalihutubia taifa Kesho Jumatatu.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.