Pata taarifa kuu
SIERRA LEONE-MAFURIKO

Mamia bado hawajulikani walipo nchini Sierra Leone baada ya maporomoko ya ardhi

Mamia ya watu bado hawajulikani walipo nchini Sierra Leone baada ya maporomoko ya ardhi na mafuriko makubwa kusababisha zaidi ya watu 300 kupoteza maisha jijini Freetown.

Madhara ya maporomoko ya ardhi na mafuriko jijini Freetown nchni Sierra Leone
Madhara ya maporomoko ya ardhi na mafuriko jijini Freetown nchni Sierra Leone STR / Society 4 climate change communication Sierra Leone / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Ernest Bai Koroma ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa na wahisani kujitokeza kuwasaidia maelfu ya watu walioathiriwa na maporomoko hayo ya ardhi.

Serikali inasema kuwa wasiwasi wa kuendelea kuwapata mamia ya watu ambao hawajapatikana wakiwa hai.

Hali hii inazua hofu kuwa huenda vifo vya watu waliopoteza maisha ikaongezeka.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini humo nayo imekuwa ikisema kuwa shughuli za uokozi zinakwenda taratibu na huenda ikachukua muda mrefu.

Mbali na watu, maelfu ya nyumba na mali yenye thamani kubwa imeharibika kutokana na mafuriko na maporomoko hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.