Pata taarifa kuu
DRC-UCHAGUZI

Corneille Nangaa: Muda wa kuandika wapiga kura hautaongezwa

Mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi nchini Jamhguri ya Kidemokrasia ya Congo, CENI, Corneille Nangaa amesema kuwa zoezi la kuwaandika wapiga kura linaloendelea katika baadhi ya majimbo nchini humo halitaongezewa muda ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Agosti.

Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi nchini DRC, Corneille Nangaa  Yobeluo (kushoto).
Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi nchini DRC, Corneille Nangaa Yobeluo (kushoto). MONUSCO/Alain Wandimoyi
Matangazo ya kibiashara

Bw Nangaa amewaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa kuwa amefurahishwa kuwa tume hiyo tayari imewaorodhesha wapiga kura milioni thelathini na saba kwa jumla ya milioni aroibaini na mbili wanaotarajiwa katika nchi nzima.

Wapinzani nchini humo wamesema CENI huenda ikatangaza kalenda ya uchaguzi mwishoni mwa mwezi huu, kama walivyoahidiwa na mwenyekiti wa tume hiyo.

Uchaguzi ulitakiwa kufanyika mwaka huu nchini DRC Chini ya mkataba uliokusudia kuepusha vurugu za kisiasa nchini humo baada ya rais Kabila kushindwa kuondoka madarakani mara muda wake ulipotamatika mwezi Desemba 2016.

Chini ya mkakati mpya upinzani umepanga kufanya mgomo wa kitaifa kuanzia Agosti 8 kama ishara ya kuonya kwa mujibu wa Francois Muamba kutoka upinzani.

Mnamo Agosti 20 upinzani umepanga kufanya maandamano mfululizo katika jiji kuu la kinshasa na majimbo 25.

Ikiwa rais Kabila hatatangaza tarehe ya uchaguzi hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Septemba hatatambulika tena kama rais wa nchi hiyo ifikapo Octoba 1, alieleza Muamba,wa chama cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.