Pata taarifa kuu
NIGER-USALAMA

Jeshi la Niger laua raia 14 kimakosa

Raia 14 waliuawa siku ya Jumatano Julai 5 na askari wa Niger kijijini kwenye mpaka kati ya Niger na Nigeria karibu na Ziwa Chad, eneo muhimu ambapo kundi la Boko Haram linaendesha harakati zake. Wahanga, ambao wote ni wakimbizi, walishukiwa kuwa wanajihadi.

Raia wa Niger pembezoni mwa mto Yobe, unaojulikana kwa jina la Komadougou karibu na mji wa Diffa, Juni 20, 2016.
Raia wa Niger pembezoni mwa mto Yobe, unaojulikana kwa jina la Komadougou karibu na mji wa Diffa, Juni 20, 2016. ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa serikali ya mkoa wa Diffa, Yahaya Godi, miongoni mwa waliouawa kumi na mbili ni raia wa Ngeria na wawili raia wa Niger. Watu hawa kumi na wanne, walikua wakitoka kupanda pilipili kwenye pembezoni mwa mto Komadougou, kwenye mpaka kati ya Niger na Nigeria katika eneo hilo ambako kunapatikana kijiji kidogo cha Abadam, ambako polisi ya wilaya ya Bosso imekua ikipiga doria.

Yahaya Godi alisema kuwa Abadam ni kijiji kilichopo katika eneo hatari na limetengwa kwa muda mrefu na kwamba mtu yeyote anayepatikana katika eneo hilo hutambulika kuwa mwanachama wa Boko Haram.

Askari waliwafananisha watu hao na wapiganaji wa kundi la Boko Haram. Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, viongozi wa mkoa wa Diffa walipata taarifa kama kundi la Boko Haram liko katika kijiji cha Abadam nchini Niger, kwenye mpaka kati ya Niger na Nigeria.

Waathiriwa wote wakiwa wakulima wasio na silaha zozote walikuwa katika eneo lililotengwa katika kijiji cha Abadam karibu na mpaka na Nigeria.

Maelfu ya watu wamewachwa bila makao katika eneo la Kusini mashariki la jimbo la Diffa na raia kupigwa marufuku kuzuru maeneo tofauti.

Kulikuwa na ripoti kinzani kuhusu opepersheni hiyo ya jeshi.

Jimbo la Diffa limekumbwa na misururu ya mashambulizi yanayotekelezwa na Boko Haram katika miaka ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.