Pata taarifa kuu
NIGER-BOKO HARAM-USALAMA

Boko Haram yawaua wanawake 9 na kuwashikilia wengine 37

Kundi la kigaidi la Boko Haram limewateka wanawake 37 na kuwauwa wengine tisa kwa kuwakata shingo Kusini Mashariki mwa Niger.

Boko Haram yasababisha mgogoro wa wakimbizi katika jimbo la Diffa nchini Niger.
Boko Haram yasababisha mgogoro wa wakimbizi katika jimbo la Diffa nchini Niger. irinnews.org
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zimesema kuwa utekaji nyara huo na mauaji hayo, yalitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika jimbo la Diffa.

Gavana wa jimbo hilo Laouali Mahamane Dan Dano, amethibitisha kukatwa shingo kwa watu tisa na utekaji nyara wa wanawake hao.

Aidha, amesema kuwa jeshi linaendelea na msako mkali kuatafuta wanajihadi hao ili kuwachukuliua hatua kali.

Mamia ya watu katika jimbo hilo wameyakimbia makwao wka hofu ya kuvamiwa na wanajihadi hao.

Hata hivyo, watu 219 hawakufanikiwa kutoroka huku wnegine wakiwa hawajui wako wapi.

Utekaji nyara huu na mauaji haya yamekuja baada ya Matifa matano ya Sahel kuzindua jeshi la pamoja la wanajeshi 5,000 kukabiliana na makundi hayo ya kijihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.