Pata taarifa kuu
NIGER

Niger yaanza kusikiliza kesi za watuhumiwa wa kundi la Boko Haram zaidi ya 1000

Nchi ya Niger imeanza kusikiliza kesi ya ugaidi inayowahusu zaidi ya wapiganaji elfu 1 wa kundi la Boko Haram, taarifa ya Serikali imesema.

Kiongozi wa kundi la Boko Haram, Abubakar Shekau.
Kiongozi wa kundi la Boko Haram, Abubakar Shekau. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mwendesha mashtaka mkuu Chaibou Samna ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP, kuwa kesi hiyo inahusu makosa ya ugaidi na ilianza Machi 2 mwaka huu.

Miongoni mwa washtakiwa waliofikishwa mahakamani wanatoka kwenye nchi za Niger na Mali pamoja na nchi jirani ya Nigeria ambako kundi la Boko Haram limekuwa likitekeleza mauaji ya raia toka mwaka 2009 kabla ya kuenea kwenye nchi za ukanda.

Baadhi ya watuhumiwa walikamatwa wakiwa mbioni kutekeleza shambulio kusini mwa Niger ambako nchi hiyo inapakana na Nigeria kwenye mji ambao ni ngome kuu ya wapiganaji hao.

Samna amesema kuwa kesi hii itadumu kwa miezi kadhaa na makosa mengi adhabu zake zitakuwa si chini ya kifungo cha miaka kumi jela.

Mwendesha mashtaka amesema kuwa baadhi ya watuhumiwa tayari wamehukumiwa na wengine mamia wameachiwa baada ya kukosekana kwa ushahidi.

Serikali ya Niger inasema kuwa imetoa pesa za kutosha kwa waendesha mashtaka kwenda kwenye maeneo ambayo matukio ya ugaidi yametekelezwa hasa kwenye mji wa Diffa jirani kabisa na kaskazini mwa Nigeria ambako ndio ngome ya wapiganaji hao.

Mwezi Desemba mwaka jana Serikali ilitangaza kuongeza kasi ya kushughulikia kesi hizi za watuhumiwa wa kundi la Boko Haram ambao wengi wamezuiliwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Watu wanaokadiriwa kufikia elfu 1 na 200 wanatuhumiwa kuwa na uhusiano na kundi la Boko Haram na wamekuwa wakizuiliwa toka mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.