Pata taarifa kuu
MISRI-HAKI

Mohamed Badie ahukumiwa kifungo cha maisha jela nchini Misri

Mahakama nchini Misri imemuhukumu kifungo cha maisha jela aliyekuwa kiongozi wa chama cha Muslim Brotherhood Mohamed Badie kwa makosa ya kupanga mashambulizi dhidi ya vyombo vya usalama.

Mohamed Badie, kiongozi mkuu wa Muslim Brotherhood anatuhumiwa  uchochezi wa mauaji.
Mohamed Badie, kiongozi mkuu wa Muslim Brotherhood anatuhumiwa uchochezi wa mauaji. REUTERS/The Interior Ministry/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Badie alikuwa sehemu ya kundi la watuhumiwa wengine 37 waliodaiwa kusababisha utovu wa usalama nchini humo katika maandamano yaliyofuata baada ya kuangushwa kwa utawala wa kiongozi wa kiislamu Mohamed Morsi mwaka 2013.

Mahakama imemuhukumu Badie kifungo cha maisha sambamba na Mahmoud Ghozlan aliyekuwa msemaji wa chama hicho na Hossam Abubakar aliyekuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, wamesema mawakili waliokuwa wakiwatetea.

Watuhumiwa wengine 13 wakiwemo Mohamed Soltan na baba yake Salah Soltan ambao nao walikuwa wasemaji wengine wa chama hicho walihukumiwa kifungo cha miaka mitano mitano jela.

Mahakama hiyo pia iliwaondolea mashtaka watuhumiwa wengine 21 waliokuwa wamejumuishwa kwenye kesi ya Badie akiwemo Gehad Haddad aliyekuwa msemaji wa kimataifa wa chama hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.