Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Zuma asema anaweza kujiuzulu kwa sababu hakuzaliwa na urais

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema hakuzaliwa na urais na anaweza hata kujiuzulu.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma REUTERS/Mike Hutchings/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Zuma amewaambia wafuasi wake wakati akitimiza miaka 75 siku ya Jumatano, kuwa chama chake cha ANC kinaweza kuamua kumwondoa madarakani ikiwa kinataka kufanya hivyo.

Kauli hii ya Zuma imekuja baada ya maandamano makubwa siku ya Jumatano jijini Pretoria kumshinikiza Zuma kujiuzulu baada ya kumfuta kazi aliyekuwa Waziri wa Fedha Pravin Gordhan.

Wanasiasa wa upinzani nchini humo wameendelea kushinikiza kujiuzulu kwa Zuma kwa madai ya ufisadi.

Inadaiwa kuwa alimfuta kazi Gordhan aliyeonekana kuzuia ufujaji wa fedha za umma.

Wiki ijayo, vyama vya upinzani vitawasilisha mswada bungeni ili kuwepo kwa upigaji kura wa kukosa imani na rais Zuma.

Uongozi wa chama cha ANC umesema haujaona sababu ya kumshinikiza Zuma ajiuzulu kwa sababu hajaona sababu ya kufanya hivyo.

Rais wa zamani Thabo Mbeki amewataka wanasiasa wa ANC kuangalia maslahi ya wananchi wala sio ya chama kuhusu madai dhidi ya Zuma.

Muungano wa vyama vya upinzani nchini humo COSATU, umesema kuwa unaunga mkono shinikizo za kujiuzulu kwa Zuma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.