Cazeneuve atembelea Tunisia baada kuondoka Algeria
Waziri Mkuu wa Ufaransa Bernard Cazeneuve anaendelea na ziara yake barani Afrika na siku ya Ijumaa ambapo sasa yupo nchini Tunisia.
Imechapishwa:
Ziara hii inakuja baada ya Cazeneuve siku ya Alhamisi kuzuru katika nchi jirani ya Tunisia na kukutana na Waziri Mkuu mwenzake Abdelmalek Sellal.
Cazeneuve na Abdelmalek wamekubaliana kudumisha uhusiano wa kidiplomasia, kisiasa na kiuchumi hata baada ya serikali ya sasa kuondoka madarakani.
Ufaransa inasalia kuwa taifa la kwanza linalowekeza nchini Algeria.
Kampuni 450 za Ufaransa zipo nchini Algeria na wawakezaji kutoka Paris hutumia Dola za Marekani Bilioni 2 kila mwaka katika uwekezaji wa sekta mbalimbali.
Aidha, Ufaransa pia hivi karibuni ilitangaza kundoa visa kwa wananfunzi wa Algeria wanaopenda kwenda kusoma nchini humo.
Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa ziara hii imewapa matumaini raia wa Algeria, ambao wengi wanaishi nchini Ufaransa kuwa uhusiano huu utaendelea kudumishwa.
Wagombea kadhaa wa urais nchini Ufaransa kama Emmanuel Macron na Marine Le Pen walizuru Algeria hivi karibuni na kuahidi kudumisha uhusiano kati ya mataifa haya mawili.
Ufaransa ilikuwa koloni ya Algeria.