Pata taarifa kuu
DRCONGO - SIASA

Rais Joseph Kabila kulihutubia taifa kupitia mabaraza ya Bunge na seneti

Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Kabange, anataraji kulihutubia taifa hii leo kupitia Bunge na Seneti, hotuba ambayo inasubiriwa na wengi kutuliza joto la kisiasa katika kipindi hiki cha mkwamo wa utekelezwaji waji wa Mktaba wa kisiasa wa Desemba 31.

Rais wa DRC, Josephu Kabila,
Rais wa DRC, Josephu Kabila, DR
Matangazo ya kibiashara

Juzi jumatatu na jana Jumanne, rais Joseph Kabila amekutana na pande mbalimbali za kisiasa katika nyakati tofauti kujaribu kuleta uwiano baina ya pande hizo na hatimaye kupatia suluhusu maswala yote yanayo leta utata hadi leo katika utekelezwaji wa Makubaliano hayo.

Wakati upinzani ukiitisha mgomo hapo jana, rais Kabila amewapokea katika nyakati tofauti viongozi mbalimbali wa kisiasa wakiwemo Kengo wa Dondo spika wa baraza la seneti, Marie Madelene Kalala, wa mashirika ya kiraia na Vital Kamerhe mwenyekiti wa chama cha upinzani cha UNC.

Baada ya kukutana na rais Kabila hapo jana Mwenyekiti wa chama cha UNC Vital Kamerhe amebaini maskitiko yake kuona lengo la makubaliano hayo linakwepeshwa ambalo ni kuelekea kwenye uchaguzi badala yake maslahi ya ugavi wa madaraka ndio yanayopewa nafasi kwa sasa.

Kamerhe amewataka wanasiasa wa nchi hiyo kutoendelea kutia mbele maslahi yao binafasi katika kutaka vyeo mbalimbali badala yake amesema muhimu ni kuhakikisha uchaguzi unafanyika.

Hapo jana shughuli zimeonekana kuzorota katika baadhi ya miji ukiwemo mji mkuu Kinshasa kufuatia wito wa upinzani kuwataka wananchi kusalia majumbani huku shughuli zikiendelea kama kawaida katika miji ya mashariki hususan Kisangani na Goma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.