Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Kadinali wa Kanisa Katoliki nchini DRC awataka wanasiasa kuheshimu mkataba wa kisiasa

Kadinali wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Laurent Monsengwo, anawataka wanasiasa nchini humo kuonesha utayari wa kutekeleza mkataba wa kisiasa uliotiwa saini mwaka uliopita.

Maaskofu wa Kanisa Katoliki DRC Kushoto ni Kadinali Laurent Monsengwo Pasinya, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu nchini humo
Maaskofu wa Kanisa Katoliki DRC Kushoto ni Kadinali Laurent Monsengwo Pasinya, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu nchini humo rfi
Matangazo ya kibiashara

Monsengwo ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kinshasa, ameongeza kuwa huu ndio wakati wa wanasiasa nchini humo kuelewa na kufahamu umuhimu wa kuiondoa DRC katika hali ya sasa ya kisiasa, ili kuandaliwa kwa Uchaguzi Mkuu mwisho wa mwaka huu.

Aidha, amewataka wanasiasa kutoka upande wa serikali na upinzani kutumia hekima na kuhakikisha kuwa, uteuzi wa Waziri Mkuu unafanyika haraka iwezekanavyo kama ilivyokubaliwa.

Tangu kifo cha kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi tarehe 1 mwezi Februari jijini Brussels nchini Ubelgiji, mazungumzo ya kutekeleza mkataba huo wa kisiasa yanaonekana kusimama.

Upinzani unasema mwili wa kiongozi wao uterejea tu nyumbani ikiwa Waziri Mkuu atateuliwa kutoka upande wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.