Pata taarifa kuu
KENYA-UN-SUDAN KUSINI

Kenya yakubali kujiunga na kikosi cha UN nchini Sudani Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa Kenya imekubali kulituma jeshi lake nchini Sudan Kusini, kwenda kujiunga na kikosi cha Umoja huo kulinda amani nchini humo.

Kikosi cha askari wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) mjini Juba,Agosti 31, 2016.
Kikosi cha askari wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) mjini Juba,Agosti 31, 2016. REUTERS/Jok Solomun
Matangazo ya kibiashara

Hatau hii inakuja miezi mitatu baada ya Kenya kuondoka nchini humo baada ya Kamanda wa Jeshi hilo ambaye ni Mkenya kufutwa kazi kwa madai ya kushindwa kulinda raia wa nchi hiyo.

Kikosi cha Kenya ambacho ni zaidia ya wanajeshi elfu moja, kinatarajiwa sasa kurejea jijini Juba baada ya mwafaka kati ya Umoja wa Mataifa na rais Uhuru Kenyatta.

Machafuko nchini Sudan Kusini yamesababisha maefu ya raia kupoteza maisha na wengine kuyahama makaazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.