Pata taarifa kuu
GAMBIA-SIASA

Wakili wa Jammeh aenda Mahakamani kuzuia kuapishwa kwa Adama Barrow

Wakili wa rais wa Gambia Yahya Jammeh, amekwenda katika Mahakama ya Juu kuzuia uwezekano wa kuapishwa kwa rais mteule Adama Barrow tarehe 19 mwezi huu.

Rais wa Gambia Yahya Jammeh
Rais wa Gambia Yahya Jammeh REUTERS/Carlos Garcia Rawlins/Files
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja wakati huu, rais Jammeh akiendelea kusisitiza kuwa hataondoka madarakani kwa madai kuwa Uchaguzi wa Desemba mwaka uliopita, haukuwa huru na haki.

Aidha, rais Jammeh amewasilisha kesi katika Mahakama ya Juu kutaka matokeo ya Uchaguzi huo yafutwe, lakini Mahakama hiyo imeahirisha kesi hiyo hadi mwezi Mei baada ya kukosekana kwa Majaji wa kuisikiliza.

Viongozi wa Muungano wa nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Kimataifa kwa pamoja wamendelea kushinikiza kuondoka madarakani kwa Jammeh.

Wabunge wa Nigeria, nao wamemtaka rais wao Muhamadu Buhari anayeongoza mazungumzo ya kumtaka Jammeh kukubali kuondoka madarakani, akubali Jammeh apewe hifadhi ya kisiasa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.