Pata taarifa kuu
GHANA-UCHAGUZI

Nana Akufo Addo ashinda kiti cha uraisi Ghana

Kiongozi wa Upinzani nchini Ghana Nana Akufo Addo ameshinda kiti cha uraisi katika uchaguzi mkuu uliofanyika juma lililopita nchini humo.

Nana Akufo-Addo ameshinda kiti cha uraisi nchini Ghana
Nana Akufo-Addo ameshinda kiti cha uraisi nchini Ghana REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Raisi wa Ghana aliyekuwa akitetea wadhifa wake katika uchaguzi mkuu amekubali kushindwa siku mbili baada zoezi la uchaguzi nchini humo kutamatika na kumpigia simu ya pongezi kiongozi wa upinzani aliyeibuka mshindi Nana Akufo-Addo.

Baada ya dalili za ushindi kuelekea upinzani kuonekana wafuasi wake tayari walikusanyika nje ya makazi ya Addo.

Kwa mujibu wa AFP,Kiongozi wa chama cha raisi anayemaliza muda wake NDC George Lawson amethibitisha raisi huyo kukubali kushindwa huku msemaji wa chama cha Upinzani NPP Oboshie Sai Cofie nae akikiri kuwa Akufo amepokea simu ya pongezi kutoka kwa raisi John Mahama.

Nana Akufo-Addo mwenye umri wa miaka 72 wakili na mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu ameibuka na ushindi wa asilimia 53.8 ya kura zote kwa ,mujibu wa tume ya uchaguzi nchini Ghana.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.